GARI LILILOBEBA KONTENA LASABABISHA AJALI MBAYA NA KUUWA WATU - AMANI ROUND ABOUT
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2025-11-21
Просмотров: 16222
Описание:
Gari lililobeba kontena limesababisha ajali mbaya katika maeneo ya Amani Round About, Wilaya ya Mjini Unguja, usiku wa tarehe 21 Novemba 2025 majira ya saa 2.
Kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa kuwa ni kufeli kwa breki za gari hilo, na kusababisha kupoteza mwelekeo kabla ya kuparamia vyombo vingine vya usafiri na watembea kwa miguu. Inasadikika kuwa watu kadhaa wamepoteza maisha, ingawa idadi kamili bado haijathibitishwa na mamlaka husika.
Vyombo vya ulinzi na usalama vimewasili eneo la tukio kwa ajili ya kutoa msaada wa dharura, kufanikisha uokozi na kuanza uchunguzi wa kina kuhusu chanzo kamili cha ajali hiyo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: