TUKIO LA WANAFUNZI KUCHEZEA MBWA NUNGWI LAZUA MJADALA, WIZARA YACHUKUA HATUA
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-02-26
Просмотров: 2803
Описание:
Kufuatia kusambaa kwa picha zinazoonesha wanafunzi wa Zanzibar Hope School wakimchezea mbwa, tukio hilo limezua mjadala mkubwa katika jamii kutokana na kugusa mila, desturi na maadili ya Mzanzibari.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Wizara ya Elimu Mkoa wa Mjini Magharibi, Naibu Katibu Mkuu Utawala wa Wizara ya Elimu Zanzibar, Amosi John Enock, amesema wizara inakemea kitendo hicho na tayari imeanza kuchukua hatua za kisheria na kiutawala dhidi ya tukio hilo, ikiwemo kuifuatilia kwa kina skuli husika. Aidha, ameomba radhi kwa jamii kutokana na taharuki iliyojitokeza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Mali Zanzibar (BPRA), Ndg. Khamis Juma Khamis, amesema kampuni inayohusishwa na tukio hilo imesajiliwa kisheria kwa ajili ya huduma za chanjo kwa mbwa, usafirishaji wa wanyama na malezi, huku akisisitiza kuwa usajili wake uko halali kwa mujibu wa taratibu.
Naye mmiliki wa skuli hiyo, Ndg. Juma Khatib Ali, ametanguliza kuomba radhi kwa jamii na kufafanua kuwa lengo la zoezi hilo lilikuwa kuwafundisha wanafunzi namna ya kuishi na mbwa kwa ustaarabu, ili kuepuka vitendo vya kuwaonea au kuwapiga mawe wanapowaona mitaani.
#ASAMOnlineTV
#ElimuZanzibar
#Nungwi
#MaadiliYaJamii
#HabariZaLeo
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: