BASATA YATOA WITO KWA WASANII KUELEKEA TAMASHA LA 17 LA MUZIKI WA CHIGOGO CHAMWINO IKULU.
Автор: WASHINDI MEDIA
Загружено: 2026-02-27
Просмотров: 62
Описание:
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limetoa wito kwa wasanii wote nchini kujirasimisha rasmi ili waweze kutambulika kisheria na kunufaika na fursa mbalimbali zinazotolewa na serikali, likisisitiza kuwa mfumo wa usajili unapatikana mtandaoni kupitia kiungo cha sanaa.go.tz.
Wito huo umetolewa leo Februari 27, 2026 katika wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma, na Afisa Sanaa kutoka BASATA, Angela Mhilu, wakati wa semina ya viongozi wa makundi yatakayoshiriki Tamasha la 17 la Muziki wa Chigogo litakalofanyika Julai 24–26, 2026 katika viwanja vya Kituo cha Sanaa na Utamaduni Chamwino (CAC).
Angela amesema BASATA imehudhuria semina hiyo kufuatia mwaliko wa CAC kama mdau muhimu wa sanaa nchini, kwa lengo la kutoa elimu kuhusu masuala matatu muhimu ambayo ni urasimishaji wa kazi za sanaa, uandishi wa maandiko ya miradi ya kisanaa, pamoja na mwongozo wa maadili katika utayarishaji wa kazi za sanaa.
“Ni muhimu kwa wasanii kujirasimisha ili kusaidia hata serikali yetu sikivu chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwa na takwimu sahihi za wasanii,”
“Urasimishaji unarahisisha upatikanaji wa misaada ya kisheria, mikopo kupitia Mfuko wa Utamaduni, elimu ya haki miliki na fursa nyingine mbalimbali,” amesema Angela.
Ameongeza kuwa usajili ni kigezo muhimu kwa msanii kushiriki katika matamasha makubwa yakiwemo yanayoandaliwa na taasisi kama Chamwino Arts Center (CAC)
“Msanii ambaye hajajirasimisha hawezi kushiriki kikamilifu. Ni lazima jamii, nchi na taasisi zinazosimamia sanaa zikufahamu,” amesisitiza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa CAC, Naamala Samson, amesema mafunzo hayo yameandaliwa kwa viongozi takribani 60 kutoka makundi 50 yanayotarajiwa kushiriki tamasha hilo, kwa lengo la kuwaimarisha katika masuala ya uongozi, fedha na fursa zinazopatikana kupitia COSOTA na Mfuko wa Utamaduni.
“Tumeona ni vyema kuwaandaa mapema ili watimize vigezo vya ushiriki, ikiwemo kujisajili BASATA. Pia tunawapa elimu ya matumizi sahihi ya fedha, uwekaji akiba, uwekezaji na umuhimu wa kujiunga na bima za afya ili kujikinga na majanga,” amesema Naamala.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: