HABARI KUBWA KUTOKA CHAKUHAWATA! YAFICHUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WALIMU NCHINI.
Автор: WASHINDI MEDIA
Загружено: 2026-03-14
Просмотров: 147
Описание:
#serikali #subscribe #newsupdate #washindimediaupdates #africa #subscribenow #subscribemychannel #tanzania #dodoma #walima #teachers
Mwenyekiti wa Chama cha Kulinda na Kutetea Haki za Walimu Tanzania (CHAKUHAWATA), Emmanuel Herman, amesema licha ya mafanikio mbalimbali yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa chama hicho, bado walimu wanakabiliwa na changamoto kadhaa zinazohitaji kufanyiwa kazi ili kuboresha ustawi wa wanachama wake.
Akizungumza Machi 14, 2026 jijini Dodoma wakati wa kikao kazi cha viongozi wa chama kutoka wilaya mbalimbali za Tanzania Bara, Herman ameeleza kuwa baadhi ya waajiri bado hawatoi ushirikiano unaohitajika kwa chama hicho.
Alisema miongoni mwa changamoto hizo ni baadhi ya wakurugenzi wa halmashauri kutokutekeleza ipasavyo makato ya ada za wanachama waliojiunga na chama hicho, licha ya walimu hao kukamilisha taratibu zote za uanachama.
“Licha ya mfanyakazi kuwa na haki ya kisheria ya kujiunga au kuhama chama cha wafanyakazi, bado kuna baadhi ya waajiri hawatekelezi wajibu wao wa kuingiza makato ya ada za wanachama wetu,” alisema Herman.
Aidha, alibainisha kuwa chama hicho pia hakishirikishwi kikamilifu katika mabaraza ya wafanyakazi yanayofanyika katika halmashauri mbalimbali, hali inayowanyima wanachama wake uwakilishi katika majadiliano yanayohusu maslahi yao.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: