WANANDOA AMBAO MMOJA ANAMAAMBUKIZI YA HIV NA AMBAYE HANA MAAMBUKIZI WANAWEZA KUPATA MTOTO MZIMA.
Автор: IringaRRH TV
Загружено: 2025-01-15
Просмотров: 953
Описание:
Lucas Mwandi ambaye ni mfamasia na mkufunzi wa afua mbalimbali za UKIMWI na Homa ya Ini kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa amesema wanandoa ambao mmoja ni muathirika wa Virus vya Ukimwi na mwingine hana maambukizi wanaweza kupata mtoto mwenye afya njema endapo huyu mwenye maambukizi atatumia dawa vizuri kwa kufuata ushauri wa wataalam wa afya.
Lucas ameyasema hayo wakati akitoa elimu ya afya hasa katika masuala ya Ukimwi katika kituo cha Radio cha Shamba fm cha mkoani Iringa.
Hata hivyo mfamasia huyo amesema changamoto iliyopo kwasasa katika jamii ni juu ya uelewa wa elimu ya homa ya ini ambayo kwasasa inakuja kwa kasi huku maambukizi ya Virusi vya Ukimwi yakishuka.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: