RAIS SAMIA KUWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MATENKI 15 YA KUHIFADHI MAFUTA KESHO
Автор: ufmradiotz
Загружено: 2026-03-02
Просмотров: 73
Описание:
Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa matenki 15 ya kuhifadhia mafuta yenye thamani ya Shilingi bilioni 678.6 katika eneo la Kigamboni Mnadani, Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Jijini Dar es salaam Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema mradi huo ni sehemu ya mpango wa upanuzi wa Bandari ya Dar es Salaam unaolenga kuongeza ufanisi, ushindani na mchango wake katika uchumi wa taifa.
Amesema matenki hayo yatakuwa na uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 378,000 za mafuta na yatapunguza muda wa meli za mafuta kukaa bandarini kutoka wastani wa siku 10 hadi siku 3, hatua itakayoongeza ufanisi, kuvutia wawekezaji na kuimarisha usalama wa nishati.
Imeandaliwa na @rajjmsangi
#UFMUpdates
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: