MIAKA MITANO YA MAFANIKIO YA LUKIZA AUTISM FOUNDATION (2020-2025)
Автор: Lukiza Autism Foundation
Загружено: 2026-02-09
Просмотров: 22
Описание:
Matokeo chanya yaliyochochewa na kazi za Lukiza Autism Foundation nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano ya kazi zake (2020-2025)
Uelewa wa Usonji
• Imeweza kufikia Takriban 30% (milioni 20+) ya Watanzania kupata elimu kuhusu Usonji
• Watanzania 15,000+, Wanufaika wa moja kwa moja wa elimu ya Usonji kupitia mbio ya Run 4 Autism Tanzania Half Marathon na Autism Awareness Charity Gala Dinner.
• 40+ Waandishi wa habari wamepata mafunzo ya uandishi jumuishi kupitia mradi wa internews in Tanzania
Elimu ya Taaluma na Mitaala zilizochochewa kuanzishwa
• Fani 4 za afya ya akili na huduma za utengamao zilizochochewa kuanzishwa MUHAS
• 250+ - Wanafunzi wanaosoma (MUHAS) kwenye fani hizi
Huduma za Utengamao
• 54 - Watoto waliopata huduma za kitabibu na utengamao kupitia mradi wa Msimbazi Mseto Autism Intervention Therapy
• 50+ Wazazi/walezi waliopata msaada wa kisaikolojia na mafunzo ya ulezi
Ugunduzi wa Mapema wa Usonji kupitia mradi wa Ustawi kwa Kila Mtoto- Viashiria vya Usonji
• 60+ Walimu wa shule za awali na walezi waliopata mafunzo haya
• 10 - Watoto waliogunduliwa mapema
Uwezeshaji wa Vijana
• 30+ Kuunga mkono kihali na kimali kituo cha @saltvtc katika kuwawezesha Vijana wenye Uhitaji maalum kupata mafunzo ya ufundi stadi
Sera na Kutambuliwa Kitaifa
• 4 - Kushiriki katika Michakato ya kitaifa (Elimu Jumuishi, Afya ya Akili, Sensa ya Watu,
Kupelekea Siku ya Usonji Duniani kuanza kuadhimishwa kitaifa nchini.
• 10 - Tuzo za kitaifa na kimataifa ikiwemo Tuzo ya Ubalozi wa afya ya akili kutoka Wizara ya Afya.
Miradi na Ushirikiano
• 5 - Miradi mikubwa ya kijamii iliyotekelezwa
• (100+)- Ushirikiano na Serikali, NGOs, vyuo, shule na sekta binafsi
Usawa wa Kijinsia
• 60% - Wanawake katika uongozi wa @lukiza_autismtanzania
• 70% Wanawake miongoni mwa wanufaika wa miradi yake
#usonji #tanzania #ustawikwakilamtoto #autismgaladinner2026 #autism
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: