🔴LIVE: MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA MAJAJI WANAWAKE (TAWJA)
Автор: MAHAKAMA YA TANZANIA
Загружено: 2026-03-10
Просмотров: 214
Описание:
Tarehe 10 Machi ya kila mwaka, Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA)
huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Majaji Wanawake. Siku hii ambayo inaadhimishwa duniani
kote, ilianzishwa rasmi na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kupitia Azimio Namba 75/274
la Aprili, 2021.
Lengo la maadhimisho haya ni kutambua mchango wa Majaji Wanawake duniani na kuhimiza
usawa wa kijinsia katika Mhimili wa Mahakama.
Kwa mwaka huu, maadhimisho haya yatafanyika siku ya Jumanne tarehe 10 Machi, katika
ukumbi wa New Generation, uliopo Kisasa, mkoa wa Dodoma na yatahudhuriwa na Wanachama
wa TAWJA ambao ni Majaji na Mahakimu kutoka mikoa mbalimbali Tanzania Bara na Visiwani.
Aidha, wadau kutoka Taasisi mbalimbali za ndani na Kimataifa kama vile UN WOMEN, Wizara ya
Katiba na Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Ofisi ya Taifa ya Mashtaka (NPS),
RITA pamoja na asasi mbalimbali za kiraia wanatarajiwa kushiriki katika maadhimisho haya.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho haya anatarajiwa kuwa, Mhe Dkt. Zuberi Homera (Mb),
Waziri wa Katiba na Sheria.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu Kimataifa ni; “Women Judges Within and
Beyond the Judiciary: Ensuring Equal Access to Justice .
”
Kwa upande wa TAWJA, maadhimisho haya yanaambatana na Kauli mbiu inayosema; “Kutoka
katika kuta za Mahakama hadi kwenye Jamii: Majaji Wanawake wakiongoza
mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.” ( From Court room to community: Women Judges
championing protection against gender-based violence) .
Ni mategemeo yetu kuwa tutakuwa pamoja katika kuadhimisha siku hii na kuendeleza
mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: