HECHE AIBUKA MAHAKAMANI NA SAKATA LA KUUAWA KWA MFANYABIASHARA WA ARUSHA, ALIANZA HIVI
Автор: WATETEZI TV
Загружено: 2026-02-20
Просмотров: 1354
Описание:
Makamu mwenyekiti taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema John Heche ameibuka mahakamani katika kesi ya Lisu na suala la kupotea na kuuawa kwa mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite Abdilah Musa maarufu Banjo .
Baada ya kuwasili chumba cha mahakama kuu masjala ndogo ya Dar es salam ambapo kesi ya uhaini dhidi ya Lisu inasikilizwa , kabla ya kesi kuanza alisalimiana na wafuasi wake kisha kuwauliza kama wana taarifa za tukio la mfanyabiashara huyo.
Mapema 19 Feb 2026 Familia ya mfanyabiashara huyo mkazi wa Sanawari Arusha Abdilah Musa maarufu Banjo iliripoti kupatikana kwa mwili wake huko wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma siku chache baada ya kuchukuliwa na wasiojulikana akiwa mkoani Arusha .
Familia ilidai kuupata mwili huo katika kijiji Bereko Kondoa ukiwa umeharibika.
Kwa mujibu wa mtoto wake , Mussa Abdilah walipigiwa simu kwamba kuna mwili wa mtu aliyekufa umekutwa pembezoni mwa barabara maeneo ya Bereko Kondoa ambapo walifika na kuthibitisha kuwa ni mwili wa mfanyabiashara huyo ambao ulikuwa umetobolewa macho na kuvunjwa mkono.
Kijana huyo Mussa alisema baba yake mzazi mnamo February 12, 2026 alikwenda kwenye mazoezi ya mwili (Gym) katika eneo la jengo la Ngorongoro lakini walikuja watu wakamchukua na kuondoka naye ambapo ndugu walimtafuta bila mafanikio mpaka hapo taarifa za kupatikana kwa mwili wake zilipotoka.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: