“KAZI KUCHART UMBEA NA KUULIZIA MASLAHI BINAFSI” WAZIRI MKUU MWIGULU ACHARUKA
Автор: WATETEZI TV
Загружено: 2026-02-20
Просмотров: 57
Описание:
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekerwa na vitendo vya baadhi ya watumishi wa umma kutochukulia kwa uzito malalamiko ya wananchi sambamba na kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo, akisema tabia hiyo inakwamisha juhudi za Serikali katika kuwahudumia wananchi.
Dkt. Nchemba ametoa kauli hiyo akizungumza na wananchi wa Moshi baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo cha Mabasi cha Ngangamfumuni, ambapo alieleza kutoridhishwa na mwenendo wa baadhi ya watumishi wanaopuuzia changamoto za wananchi badala ya kuzitatua kwa wakati.
Amesema baadhi ya watumishi wamekuwa wakifanya kazi kwa kuangalia maslahi yao binafsi badala ya kutanguliza maslahi ya umma, hali ambayo ni kinyume na maadili na wajibu wao wa msingi katika utumishi wa umma.
Waziri Mkuu alisisitiza kuwa Serikali haitavumilia uzembe, uvivu na vitendo vinavyokwamisha utoaji wa huduma kwa wananchi, na kuwataka watumishi wote kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uwajibikaji ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi.
Aidha, alieleza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati, huku akiwataka viongozi na watumishi wa umma kusikiliza na kushughulikia kero za wananchi kwa haraka ili kuimarisha imani yao kwa Serikali.
Ametoa kauli hiyo katika Ziara ya siku nne mkoani Kilimanjaro ambayo ni sehemu ya ratiba yake ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, kusikiliza changamoto za wananchi na kufuatilia utendaji wa watumishi wa umma katika maeneo mbalimbali
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: