DED LUDEWA APONGEZA USHIRIKIANO UJENZI WA KITUO CHA AFYA MAWENGI.
Автор: LUDEWA ONLINE TV
Загружено: 2026-02-15
Просмотров: 90
Описание:
DED LUDEWA APONGEZA USHIRIKIANO UJENZI WA KITUO CHA AFYA MAWENGI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Sunday Deogratias, ameipongeza kamati ya ujenzi wa Kituo cha Afya Mawengi kwa ushirikiano mzuri uliofanikisha utekelezaji bora wa mradi huo muhimu wa huduma za afya.
Pongezi hizo zimetolewa wakati wa ziara ya Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ludewa iliyolenga kukagua maendeleo ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa wilayani humo, ikiwemo ujenzi wa kituo hicho cha afya.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi amesema mradi huo ukikamilika utakuwa na mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa eneo husika. Amesema uamuzi wa kuwashirikisha wananchi katika usimamizi wa mradi unalenga kujenga umiliki wa mradi huo kwa jamii. Ameongeza kuwa kamati ya ujenzi ya Mawengi inaweza kuwa mfano bora wa usimamizi wa miradi mingine ya maendeleo wilayani humo.
Katika ziara hiyo, Kamati ya Siasa ya CCM ilitembelea pia miradi mingine ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa madarasa saba, mabweni matatu na matundu 16 ya vyoo katika Shule ya Sekondari Ulayasi, ujenzi wa shule mpya ya Amali katika shule hiyo, ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje katika Kituo cha Afya Madope pamoja na mradi wa maji Madope. Kamati hiyo imeeleza kuridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa miradi hiyo na kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.
Aidha, mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Mawengi unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi milioni 250 fedha kutoka Serikali Kuu
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: