BARABARA YA MISIGIRI–NKINGI YALETA NAFUU KWA SHUGHULI ZA KIUCHUMI
Автор: CALES TV
Загружено: 2026-02-26
Просмотров: 112
Описание:
IRAMBA – SINGIDA
Wananchi wa Kijiji cha Misigiri, Kata ya Ulemo, Kitongoji cha Miembeni, wameipongeza Serikali kwa ujenzi wa barabara ya lami inayounganisha barabara kuu ya Misigiri kuelekea Kijiji cha Nkingi.
Wakizungumza na waandishi wa habari waliotembelea eneo la mradi huo, wananchi wamesema barabara hiyo imeanza kuleta nafuu kwa shughuli za kiuchumi, kwani usafiri na usafirishaji sasa unafanyika kwa urahisi zaidi.
Hata hivyo, wameeleza changamoto ya maji ya mvua kuingia katika makazi yao na kuiomba kampuni ya mkandarasi, Saimoo Co. Ltd, kujenga mitaro ili kuzuia maji hayo yasiharibu makazi.
Aidha, wananchi hao wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi na Waziri Mkuu, Mwigulu Nchemba, kwa kusimamia upatikanaji wa barabara hiyo, huku wakiiomba Serikali kuwafikiria wananchi waliopata athari wakati wa ujenzi ili waweze kufidiwa.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: