SIRI 5 KUANZA NA KUFANIKIWA KWENYE KITU CHOCHOTE KWENYE MAISHA (Safari ya NDOTO zako)
Автор: LENZI | Michael Kamukulu
Загружено: 2025-02-05
Просмотров: 4881
Описание:
Kila mtu anatamani kuanza lakini sio wote wanapiga hatua ya ujasiri na kuanza safari ya ndoto na mafanikio yako. Na wachache walifanikiwa kuanza, wanaanguka na kushindwa kuamka na kuanza upya.
Kuna siri 5 zinazoweza kukusaidia kuanza au kuanza upya na kufanikiwa kwenye kitu chochote unachotamani kufanya kwenye maisha yako. Ndoto yoyote haiwezi kutimia kabla ya kuamka na kuanza kuifanyia kazi kwa hatua halisi. Jiunge na Michael Kamukulu kupitia @lenzi.michaelkamukulu ili uweze kujifunza jinsi ambavyo siri hizi zinaweza kukuondolea na kukusaidia kuishinda hofu ya kuanza au kuanza upya. Acha kuogopa, inuka upige hatua ya ujasiri na uziendee ndoto zako za maisha ya mafanikio; usisubiri hali iwe nzuri na rahisi. Hatua ya kwanza unayochukua leo ndiyo inayokupeleka kwenye mafanikio.
Jifunze jinsi ya kuwa mtu wa tofauti, na upate fursa na nafasi ya kuinuka na kusimama imara ukiwa kiongozi na mwongoza njia wa maisha yako na kuwa na ushawishi kwa watu wengi. Pata maarifa na ujuzi utakaokubadilisha na kuwa na tabia za watu wenye mafanikio na matokeo makubwa kifedha na kimaisha kwa ujumla. Ni wakati wako kung'ara na kuwa mtu wa thamani zaidi kwa wengine na kwa maisha yako. Utajiri na umasikini vyote viko kwenye nguvu ya tabia, mienendo na maamuzi yako ya kila siku.
Kwenye video hii utajifunza mbinu na siri 5 za kuanza au kuanza upya safari yako ya mafanikio katika maisha.
01. Anzia hapo ulipo
Usingojee mpaka upate mazingira bora, mtaji mkubwa au maarifa yote. Anza na kile unachoweza kufanya sasa hivi. Hata kama ni hatua ndogo, inakukaribisha kwenye safari ya maendeleo.
02. Anza na hicho ulichonacho
Huna kila kitu, lakini una kitu cha kuanzia. Una maarifa, vipaji, muda, simu, au hata marafiki wanaoweza kukusaidia. Usitafute visingizio—tumia rasilimali zilizopo kwa ubunifu.
03. Anza bila kujali waliokutangulia
Watu wengi huchelewa kuanza kwa sababu wanaogopa ushindani au kuona wengine wamefanya makubwa. Kumbuka, kila mtu ana safari yake. Usijilinganishe—anza safari yako bila hofu.
04. Usijali safari ya mtu mwingine
Wengine wanaweza kuanza baada yako na wakafanikiwa haraka, lakini hiyo haimaanishi umeshindwa. Kila mtu ana mwendo wake. Jifocus kwenye maendeleo yako binafsi badala ya kulinganisha maisha yako na ya wengine.
05. Yakubali mapungufu yako na anza nayo hivyo hivyo
Huwezi kuwa mkamilifu mwanzoni, na hiyo ni sawa. Safari yako itakufundisha, utakua, na hatimaye utakuwa bora zaidi. Usikubali hofu ya kutokamilika ikuzuie kuanza—anza, jifunze, na endelea mbele!
Mafanikio yako yanategemea hatua unayochukua leo. Hivyo, usisubiri kesho—ANZA SASA
🔔 Usisahau:
✔️ Ku-like, ku-subscribe, na kushare video hii na wengine!
✔️ Kuweka maoni yako—ni ipi mbinu inayokuvutia zaidi?
———————————————
Wasiliana nasi kwa huduma zaidi ikiwemo:
1. Mafunzo na mwongozo maalum wa kufikia malengo (personal/individual coaching)
2. Mafunzo na mwongozo maalum kwa makundi na taasisi (group coaching)
3. Ushauri wa kitaalam kuhusu maendeleo binafsi (personal development)
Mawasiliano yetu:
Simu: +255 752 465 039
Baruapepe: [email protected]
* *
Pata Kozi Kuhusu jinsi ya kujiajiri na kuongeza kipato kwa kutumia MAUDHUI kwa bei nafuu ya TZS 15,000 tu kupitia hapa https://tr.ee/UTrb-ghbfk
#HatuaMojaMbeleKilaSiku #michaelkamukulu #lenzimindset #lenziacademy
Chapters
00:00 Safari ya ndoto zako
00:38 1. Anzia hapo ulipo
02:00 2. Anza na hicho ulichonacho
02:45 3. Anza bila kujali waliokutangulia
03:45 4. Usijali safari ya mtu mwingine
04:48 5. Anza na mapungufu yako
07:03 Closing
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: