CHEKECHE | Kipi kitainusuru Mashariki ya Kati?
Автор: Azam TV
Загружено: 2026-03-15
Просмотров: 1537
Описание:
Zilianza saa 24 za mashambulizi, lakini sasa zimepita wiki mbili bila dalili ya kusitishwa kwa vita kati ya Iran na Israel, huku eneo la Mashariki ya Kati kwa ujumla likiendelea kushuhudia mvutano na kauli kali kutoka kwa viongozi wa pande zote.
Msimamo wa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ni kudhamiria kuuondoa madarakani utawala wa viongozi wa kidini wa Iran; wakati Kiongozi Mkuu mpya wa Iran, Mojtaba Khamenei, akiwataka majirani wa nchi yake kufunga kambi za kijeshi za Marekani.
Dunia sasa ipo njia panda kutokana na hali hiyo inayoendelea. Katikati ya mzozo huu unaozua taharuki kwa mataifa mengi, swali linalobaki ni: ni nini kitakachoinusuru Mashariki ya Kati?
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: