UONGOZI WA SKULI YA ZANZIBAR HOPE WAKUTANA NA WAZAZI KUJADILI TUKIO LA WANAFUNZI NA MBWA
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-03-11
Просмотров: 361
Описание:
Hivi karibuni kumekuwa na picha zilizosambaa mitandaoni zikionyesha wanafunzi wa Skuli ya Zanzibar Hope wakimchezea mnyama aina ya mbwa, tukio lililozua mjadala mkubwa katika jamii na kuibua taharuki hususan kwa Wizara ya Elimu Zanzibar.
Kutokana na tukio hilo, mamlaka husika ziliitisha mkutano na waandishi wa habari pamoja na Business and Property Registration Agency (BPRA) ili kutoa ufafanuzi kuhusu suala hilo na hatua zilizochukuliwa.
Leo, Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Zanzibar Hope, Ndugu Chacha Joseph John pamoja na Mkurugenzi wa skuli hiyo, Ndugu Juma Khatib Ali wamefanya kikao na wazazi kwa lengo la kujadili na kulikemea tukio hilo.
Katika kikao hicho, uongozi wa skuli umekanusha baadhi ya taarifa zilizokuwa zimeandikwa katika waraka uliosambaa mitandaoni, ikiwemo madai kwamba skuli hiyo haina mwalimu wa Kiislamu. Aidha, waliwaomba wazazi kutoa ufafanuzi kuhusu yaliyomo kwenye waraka huo ili kupata ukweli na kuweka uwazi wa taarifa kwa jamii.
Kwa upande wao, wazazi wamesema ni muhimu kwa pande zote kushirikiana ili kuweka mikakati ya maendeleo na malezi bora kwa wanafunzi. Pia wameuomba uongozi wa skuli kuunda kamati ya maadili kufuatia tukio hilo ili kuhakikisha mwenendo mzuri wa wanafunzi unaimarishwa.
#ASAMOnlineTV
#ElimuZanzibar
#ZanzibarHopeSchool
#MaadiliYaJamii
#Zanzibar
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: