TRA YAFIKA HADI GEREZANI, HOSPITAL YA WAGONJWA WA AKILI, SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-03-11
Просмотров: 508
Описание:
Waswahili wanasema “fadhila si mali, bali ni moyo.” Na pale moyo unapoguswa na huruma ndipo utu wa kweli hujitokeza. Katika kuadhimisha International Women's Day, Tanzania Revenue Authority (TRA) imeonesha mfano wa kuigwa kwa kugusa maisha ya wanawake waliopo katika mazingira magumu.
Kupitia ziara maalum ya kijamii, TRA ilitoa msaada wa vifaa mbalimbali na kuwatembelea wanawake wagonjwa wa akili pamoja na watoto na pia kuwafikia wafungwa wanawake, hatua iliyolenga kuwapa faraja, matumaini na kuwahakikishia kuwa jamii bado inawajali.
Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mgeni Hassan Juma, aliyekuwa mgeni rasmi. Akizungumza katika hafla hiyo aliipongeza TRA kwa hatua hiyo, akisema jamii inahitaji zaidi vitendo vya huruma na mshikamano kama hivyo.
Amesema maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hayapaswi kuwa sherehe pekee, bali pia ni fursa ya kutafakari nafasi ya mwanamke katika jamii na namna ya kumuinua zaidi. Alisisitiza kuwa mwanamke ni uti wa mgongo wa familia na jamii, na pale anapothaminiwa na kupewa nafasi, maendeleo ya taifa huimarika.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: