PROF.MBARAWA ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA CATC, ASISITIZA UBORA NA KUAKISI THAMANI YA FEDHA
Автор: Tanzania Civil Aviation Authority - TCAA TV
Загружено: 2026-03-04
Просмотров: 111
Описание:
Waziri wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa Machi 04, 2026 alifanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi wa majengo ya Chuo cha Usafiri wa Anga (CATC) katika eneo la Banana, jijini Dar es Salaam na kusisitiza umuhimu wa mradi huo katika kuimarisha sekta ya usafiri wa anga nchini.
Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo,Prof.Mbarawa alisema ameridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao mpaka sasa Ujenzi wake uko ndani ya muda na unaendelea kwa kasi inayotakiwa na katika ubora, ratiba, viwango vya kitaalamu na thamani halisi ya fedha I ikizingatiwa.
Aliongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita imefanya mambo makubwa kwenye sekta ya anga ikiwemo ujenzi na uboreshaji wa viwanja vya ndege karibu kila mkoa, ununuzi wa ndege na sasa imejipanga kuendelea kuimarisha miundombinu ya mafunzo ya sekta ya anga ili kuzalisha wataalamu wenye ujuzi wa hali ya juu watakaokidhi mahitaji ya soko la ndani na kimataifa.
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania ni taasisi ya umma yenye jukumu la kudhibiti sekta ya usafiri wa anga katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mamlaka iliundwa kwa Sheria ya Usafiri wa Anga, Sura ya 80 (R.E 2006).
Majukumu ya kisheria ya Mamlaka ni kudhibiti masuala ya ki-usalama, ki-uchumi katika usafiri wa anga na kutoa huduma za uongozaji ndege.
Pia Mamlaka inatoa huduma za uongozaji ndege kwenye vituo vya ndege kumi na nne (14) ambavyo ni: Dar es Salaam, Kilimanjaro,Tanga, Arusha, Mwanza,Tabora,Kigoma, Dodoma, Iringa, Songwe, Songea, Mtwara, Zanzibar na Pemba
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: