NENO LA SIKU | Luka 12 | Maombi Ya Toba Kwa Dhambi Za Siri | Isaac Javan
Автор: Neno La Siku
Загружено: 2024-06-13
Просмотров: 5782
Описание:
Leo tunasoma kitabu cha Luka sura ya kumi na mbili, na tunaenda kufanya maombi ya toba kwa dhambi za siri. Lengo la maombi ya leo ni kufungua njia za kiroho ili tuweze kujibiwa maombi yetu.
Dhambi inapofanyika inaweka kizuizi cha maombi katika ulimwengu wa roho. Watu wengi maombi yao yamezuiliwa kwa sababu ya dhambi. Lakini dhambi tunayokwenda kuitubia siku ya leo, ni dhambi ya siri.
Yapo mambo yanafanyika kwa siri bila watu kujua, na shetani anayasimamia na kuyatumia dhidi yetu. Katika somo la leo utajifunza dhambi ya siri ni ipi, na pia utajifunza tafsiri mbalimbali za dhambi ya siri, ili zikupe upana wa maarifa ya kujiombea wewe mwenyewe.
Nakutakia ushindi mkuu kwenye maombi ya leo. Mungu akutane na wewe kupitia maombi haya. Nakuombea ukamuone Mungu akikuvusha na kukupa ushindi. Yale yote yaliyokuwa hayawezekani yakaanze kuwezekana kwako. Damu ya YESU ikutangulie kwenye maombi ya leo, na BWANA akupe kibali, neema, ushindi, na maisha mapya ndani yake. Mungu akubariki sana. Amen!
Isaac Javan
+255 745 76 45 72
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: