NENO LA SIKU | Marko 12 | Maombi Ya Kushinda Roho Inayozuia Ushindi Wako | Isaac Javan
Автор: Neno La Siku
Загружено: 2024-04-19
Просмотров: 8227
Описание:
Leo tunasoma kitabu cha Marko sura ya kumi na mbili, na tunaenda kufanya maombi ya kushinda roho inayozuia ushindi wako. Hii ni aina ya roho inayotenda kazi kuzuia mtu asipate matokeo ya maombi; lakini pia, ni nguvu ya kiroho inayomfanya mtu asiweze kupokea matokeo mazuri ya kazi yake au jitihada yake.
Ni roho ya kishetani inayotenda kazi ili kuharibu maisha ya watu. Na watu wengi wanateseka na hawajui cha kufanya. Lakini imempendeza Mungu siku ya leo tupate kuomba ili Mungu atufungue na kutuweka huru, na kutusaidia tuweze kuishi maisha ya ushindi tukiwa hapa duniani.
Katika siku ya leo, utaenda kujifunza namna hii roho inavyofanya kazi, na utajifunza kuzitambua dalili zake, ili ikupe wepesi wa kujiweka tayari kufanya maombi na kuishinda ili isikuharibie maisha yako. Nami nakuombea YESU akuonekanie na kukushindia katika maombi ya leo. Nakuombea kuanzia leo uanze kupokea ushindi wako, na uanze kuvuka kwenye mambo yako yote. Damu ya YESU ikufunike, ikupiganie na kukushindia katika yote. Amen!
Isaac Javan
+255 745 76 45 72
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: