WAZIRI SHARIF ARIDHISHWA NA HALI YA BEI ZA BIDHAA UNGUJA
Автор: ASAM Online TV
Загружено: 2026-02-25
Просмотров: 1396
Описание:
Kaimu Waziri wa Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda ambaye pia ni Waziri wa Kazi na Uwekezaji, Mhe. Sharif Ali Sharif, amesema ameridhishwa na hali ya upatikanaji na bei za bidhaa katika masoko ya Unguja, akibainisha kuwa bei zimeonekana kupungua kwa kiwango kikubwa.
Amesema Wizara itaendelea kutoa elimu kwa wafanyabiashara kuhusu umuhimu wa kufuata taratibu za biashara na kuzingatia usafi wa mazingira wanayofanyia shughuli zao.
Kauli hiyo ameitoa baada ya kufanya ziara ya kukagua bei za vyakula katika Soko la Darajani, Soko la Mombasa, Soko la Mwanakwerekwe pamoja na Soko la Jumbi.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani Halali wa Biashara, Ndg. Alya Emanuel Juma, amesema lengo la ziara hiyo ni kuhakikisha wafanyabiashara wanabandika bei za bidhaa zao ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa kwa wananchi.
Mkuu wa Soko la Jumbi, Faki Suleiman Hatib, ameeleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili wafanyabiashara ni upotevu wa mitaji, jambo linalohitaji ufumbuzi wa pamoja.
#ASAMOnlineTV
#BiasharaZanzibar
#MasokoYaUnguja
#BeiZaBidhaa
#UshindaniHalali
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: