WAZIRI MCHENGERWA AMUWASHIA MOTO MKURUGENZI SENGEREMA; ZAHANATI IFUNGULIWE; MBUNGE ATAMANI KULIA.
Автор: Yuboxtv
Загружено: 2023-12-18
Просмотров: 4703
Описание:
WAZIRI MCHENGERWA AMUWASHIA MOTO MKURUGENZI SENGEREMA; ZAHANATI IFUNGULIWE; MBUNGE ATAMANI KULIA.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tamisemi,Mhe.Mohamed Mchengerwa ametoa maagizo ya vituo vya afya vilivyopo wilayani Sengerema vianze kutoa huduma haraka kwa wananchi.
Akizungumza kwenye kituo cha afya kilichopo kijiji cha Kanyerere kilicho chini ya mradi wa Tasaf kilichofika asilimia 96 lakini hakijaanza kutoa huduma,Waziri Mchengerwa amesema haoni sababu ya msingi ya kuwacheleweshea huduma wananchi licha ya kupewa maelezo ambayo hayakumridhisha.
Amebainisha maelezo yote aliyopatiwa kuhusu kituo hicho yameonesha waliopewa dhamana ya kusimamia wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo hivyo ametoa wiki mbili kituo hicho na vingine 11 viwe vimeanza kutoa huduma.
"Katibu Tawala wa Mkoa nakuagiza simamia ipasavyo zoezi hili waandikie barua wahusika wote ili mradi huu uanze kazi,hatuna sababu ya kuwapa hasira wananchi wetu kituo wanakiona lakini wanaendelea kuteseka kupata huduma za afya,"Mhe Mchengerwa.
.
.
.
.
.
.
#trending #mchengerwa #mwanza #raissamia
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: