CODEPATA BORESHENI UTENDAJI KULETA MAENDELEO.
Автор: CLOUDS HABARI
Загружено: 2025-05-07
Просмотров: 47
Описание:
CODEPATA BORESHENI UTENDAJI KULETA MAENDELEO.
Serikali imekitaka chama cha wataalamu wa maendeleo ya jamii Tanzania CODEPATA, kuimarisha utendaji wa wanachama wa chama hicho ili kuweza kuleta matokeo Chanya ndani ya sekta ya maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu na kwa maslahi ya taifa.
Kauli hiyo imetolewa na naibu Waziri mkuu na Waziri wa nishati Dkt. Doto Biteko wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa wataalamu wa maendeleo ya jamii Nchini ambapo amesema serikali itaendelea kuongeza ajira kwa wataalam wa maendeleo ya jami
Aidha DKT Biteko ameongeza kuwa serikali imeendelea kufanya jitihada mbalimbali katika kuhakikisha inaanzisha mpango wa taifa wa kuhamasisha na kusimamia maendeleo kuanzia ngazi ya msingi kwa mwaka 2023/26.
Awali Waziri wa maendeleo ya jamii, jinsia, wanawake na makundi maalumu Dkt. Dorothy Gwajima ametumia fursa hiyo kuzungumzia lengo kuu la mkutano huo wa mwaka huku rais CODEPATA akielezea mikakati mbalimbali ya chama hicho
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: