TRA United kuwa timu tishio Afrika, yaundiwa bodi ya usimamizi, yumo Wilfred Kidao
Автор: Azam TV
Загружено: 2026-02-18
Просмотров: 320
Описание:
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Juma Mwenda amezindua bodi ya usimamizi wa timu ya “TRA United Sports Club” huku akiitaka kuifanya timu hiyo kuwa tishio katika ligi za ndani na kimataifa.
Pamoja na mambo mengine, Mwenda ameisisitiza bosi hiyo kusimamia nidhamu ya timu ili kuifanya kuwa ya mfano dhidi ya vilabu vingine vinayoshiriki ligi mbalimbali nchini.
Amesema dhamira ya TRA kuianzisha timu hiyo mbali na kutoa burudani imelenga kupeleka ujumbe kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa hiari jambo ambalo ndiyo msingi wa ukuaji wa uchumi wa nchi.
“….ni imani yangu nyinyi kama bodi mtakwenda kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wananchi wanaliona suala la kulipa kodi kama jukumu lao na siyo vinginevyo” amesema Mwenda.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya ‘TRA UNITED’ Edmund Kawamala, amempongeza Kamishna Mwenda kwa wazo lake la kuianzisha timu hiyo ambayo matarajio yake itakuwa kuwa moja ya timu tishio ya mpira wa miguu katika Bara la Afrika.
Amesema wakiwa kama Bodi, watahakikisha wanafanya kila linalowezekana kuiwezesha timu hiyo kupelekea ujumbe wa kulipa kodi kwa wananchi.
Mbali na Mwenyekiti wake Edmund Kawamala, wajumbe wengine wanane wanaounda bodi hiyo ni pamoja na Dkt. Wilfred Kidao, Angelina Ngalula, Juma Kisongo, Kamna Shomari, Zahoro Salum, Paul Walalaze pamoja na Elikunda Mndeme huku nafasi ya mjumbe wa mwisho ikitarajiwa kujazwa wakati wowote..
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: