MAFURIKO SONGWE YAWAKIMBIZA WAKAZI KWENYE MAKAZI YAO
Автор: ufmradiotz
Загружено: 2026-01-09
Просмотров: 201
Описание:
Wananchi wa kijiji cha Ntinga, kata ya Msangano, wilayani Momba mkoani Songwe, wamelazimika kuyahama makazi yao na kutafuta hifadhi katika maeneo ya jirani kufuatia mafuriko ya maji yaliyovamia makazi yao baada ya mvua kubwa kunyesha usiku wa kuamkia leo katika wilaya za Ileje, Mbozi na Tunduma.
Inaelezwa kuwa mafuriko hayo yaliyoanza saa 9 usiku yamesababisha maji kuzingira makazi ya wananchi, kuharibu vyakula vilivyokuwa ndani ya nyumba na kuwaacha wakazi hao bila hifadhi ya kulala usiku, licha ya maji kuanza kupungua katika baadhi ya maeneo.
Diwani wa kata ya Msangano amesema kuwa kutokana na mafuriko hayo, wananchi wako katika hatari ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko, hivyo ametoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka za kiafya na kibinadamu ili kudhibiti athari zaidi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Momba, Elias Mwandobo, ametembelea kijiji hicho kujionea hali halisi na kueleza kuwa Serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali kuhakikisha usalama wa wananchi. Aidha, amewataka wakazi hao kuwa watulivu, kushirikiana wao kwa wao wakati Serikali ikiendelea kufanya tathmini ya madhara yaliyojitokeza.
✍Joyce Lyanda
Mhariri | @rajjmsangi
#UFMUpdates
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: