MIKOA MIWILI YAPATA SEMINA ELEKEZI YA KUENDELEZA PROGRAMU YA KILIMO NA UVUVI – SINGIDA
Автор: CALES TV
Загружено: 2025-05-24
Просмотров: 57
Описание:
Na Mwandishi wetu - Singida
Mikoa ya Shinyanga na Tabora imeanza kupatiwa semina elekezi ya kuendeleza programu ya kilimo na uvuvi inayoendelea kutekelezwa nchini, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuwaongezea uwezo na uelewa juu ya afua za kilimo bora na uvuvi endelevu.
Semina hiyo inafanyika mkoani Singida, chini ya uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi, inayolenga kuongeza tija ya uzalishaji kwa wakulima na wavuvi wadogo.
Akizungumza katika mafunzo hayo, Mratibu wa Programu hiyo Iren Mbando, kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, alisema kuwa semina hiyo inalenga kuwajengea uwezo watendaji na waratibu wa mikoa hiyo kuhusu afua za kilimo na uvuvi zinavyotekelezwa kwenye maeneo husika.
“Programu hii ya kitaifa ilianza kutekelezwa mwaka 2021 na inatarajiwa kukamilika mwaka 2027, ikihusisha mikoa 11, halmashauri 41 na kata 205 kote nchini,” alisema Mbando.
Mbando alieleza kuwa programu hiyo inalenga kuwafikia walengwa zaidi ya milioni moja, ambapo semina hiyo ni sehemu ya kuongeza uelewa kuhusu matumizi ya mbegu bora kama mahindi, alizeti, dengu na maharage, pamoja na kuimarisha maarifa ya uvuvi bora kwa jamii zinazoishi karibu na vyanzo vya maji.
Alisema sababu ya kuanza na mikoa ya Shinyanga na Tabora ni kwa ajili ya kuipa nafasi ya kwanza katika kujifunza, ili wanufaika waweze kuelewa vizuri umuhimu wa teknolojia na mbinu mpya za kilimo na uvuvi wa kisasa kabla ya kufikia mikoa mingine.
“Lengo letu ni kuwawezesha wakulima na wavuvi kubadilika kutoka kilimo na uvuvi wa mazoea kwenda kwenye uzalishaji wenye tija na kibiashara,” aliongeza.
Programu hii inatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na wadau wa maendeleo, ikiwa na lengo la kuboresha maisha ya wananchi kupitia kilimo na uvuvi wenye tija, wa kisasa na endelevu.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: