BARABARA, RELI KIKWAZO MAENDELEO YA BANDARI YA KAREMA
Автор: The Katavi Independent
Загружено: 2023-03-19
Просмотров: 3074
Описание:
The Kavavi Independent || Changamoto ya miundombinu hususani ya barabara na reli kutoka Mpanda kwenda katika eneo la Bandari ya Karema iliyopo Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi imepelekea meli za mizigo kutotia nanga katika bandari hiyo.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC), Jerry Silaa, walipotembelea na kukagua utekelezaji wa mradi wa kimkakati wa Ujenzi wa Bandari ya Karema, unaotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA).
Akiongoza Kamati hiyo Mwenyekiti Silaa amesema tokea Bandari hiyo ifunguliwe rasmi septemba 2022 hadi sasa imeingiza kiasi cha shilingi milioni nne na laki nane ambazo amesema ni kiasi kidogo ukilinganisha na uwekezaji uliofanyika wa shilingi Bilioni 47.97
Amesema kukamilika kwa miundombinu hiyo itasaidia malori yanayopeleka mizigo Congo badala ya kupita njia ya Tunduma yatapita njia ya Mpanda na kwenda hadi Karema na baada ya kufika Bandari ya Karema ni rahisi kufika Bandari ya Karemii iliyopo Congo katika Jimbo la Rubumbashi.
Silaa amesema mpango wa Serikali ni kujenga barabara ya kilomita 110 kutoka Kijiji cha Kagwira hadi katika bandari ya Karema pamoja na kujenga reli kutoka Mpanda hadi Karema.
Ameishauri serikali kuongeza kasi ya ujenzi na utunzaji wa miradi hiyo kwa kuwa Bandari imekwisha kamilika kwa asilimia mia moja.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: