RC MHITA AFUNGUA MGODI WA NYANDOLWA ULIOUA BAADA YA UKAGUZI NA UKARABATI
Автор: RS Shinyanga
Загружено: 2026-02-19
Просмотров: 5
Описание:
Serikali Mkoa wa Shinyanga imeruhusu kampuni ya HHH and Partners kuendelea na uchimbaji wa madini katika eneo la Nyandolwa baada ya kusimamishwa kufuatia ajali ya Agosti 11, 2025 iliyosababisha mafundi 25 kufukiwa.
Akizungumza kwa niaba ya Serikali Leo Februari 19,2026, Mkuu wa Mkoa, Mhe. Mboni Mhita, amesema uamuzi huo umefanyika baada ya ukaguzi wa kina uliofanywa na wataalamu wakiongozwa na Mkaguzi Mkuu wa Migodi nchini.
Kati ya maduara 26 ya HHH, saba pekee yameruhusiwa kuendelea na uzalishaji huku 19 yakifungwa kutokana na sababu za kiusalama. Serikali imesisitiza wamiliki kuzingatia kikamilifu taratibu na miongozo ya usalama ili kuzuia maafa kujirudia.
Menejimenti ya mgodi imeishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuufungulia mgodi huo, ikieleza kuwa hatua hiyo itarejesha ajira na kuinua uchumi wa wananchi wa eneo hilo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: