1||SI KILA UFUNUO NI WA KUTANGAZA
Автор: Gwakisa Mwaipopo
Загружено: 2026-02-16
Просмотров: 150
Описание:
Mathayo 17:1–7 si hadithi tu ya mlima—ni ujumbe wa Mungu kwa kizazi hiki. Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana juu ya mlima, akabadilika sura; utukufu wake ukaonekana, na sauti ikatoka mbinguni: “Huyu ni Mwanangu mpendwa… msikieni yeye.”
Hii ni ishara: Mungu anawatenganisha wachache ili awaandae wengi. Anawapandisha juu kwa ufunuo, si kwa kiburi, bali kwa mizigo ya kesho. Kabla ya msalaba, kuna mlima; kabla ya mateso, kuna uthibitisho; kabla ya giza, kuna nuru ya kusema, “Huyu ndiye.”
Lakini angalia hatari: Petro alitaka vibanda. Huo ni mtego kwa watu wengi kutaka kukaa kwenye hisia za kiibada na kuigeuza kuwa makazi yasiyobadilika. Mungu hakusema “jengeni vibanda,” alisema “msikieni Yeye.” Hii inatuonesha kuwa Mungu anavunja ibada isiyo na utii. Anakataa mazoea yanayopendeza, lakini hayabadilishi maisha.
Na waliingiwa na hofu, Yesu aliwagusa akasema: “Inukeni, msiogope.” Huu ndio wito wa sasa: simama. Usitawaliwe na hofu. Usichanganye sauti ya Mungu na kelele za dunia. Ufunuo hautokuua utakuinua, na kukufanya ukitii maelekezo ya Mungu.
Leo Mungu analiambia kanisa: Acheni kutafuta ishara tu; tafuteni sauti. Acheni kuabudu kwa midomo pekee; msikieni Kristo na mfuate. Kwa sababu ufunuo wa kweli hauishii mlimani unakushusha chini uende kutenda mapenzi ya Mungu.
Msikieni Yeye.
https://distrokid.com/hyperfollow/voh...
https://distrokid.com/hyperfollow/voh...
https://distrokid.com/hyperfollow/voh...
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: