FUFUA USIKIVU WA SAUTI YA MUNGU
Автор: Gwakisa Mwaipopo
Загружено: 2026-02-03
Просмотров: 155
Описание:
“Fufua Usikivu Wako” (1 Samweli 3:1–11)
Kuna watu wengi wako karibu na mambo ya Mungu, lakini hawatambui sauti ya Mungu. Samweli alikuwa hekaluni, lakini mara ya kwanza alidhani anaitwa na Eli mpaka alipofundishwa kujibu: “Nena Bwana, kwa maana mtumishi wako anasikia.” Ndipo Mungu akamkabidhi ujumbe mkubwa.
Ujumbe wa leo ni huu: Mungu anataka usikie. Si ibada tu, si kuimba tu, si kuwa kanisani tu bali kuwa mtu wa usikivu na utii. Ukifufua usikivu wako, utaacha kubahatisha; utaanza kuongozwa.
Jiulize: sauti ya Mungu imekuwa ikikuita, lakini umeichanganya na sauti ya watu, hofu, au presha?
Karibu tusikie pamoja. Andika kwenye comment: “Nena Bwana, nasikia.”
Kisha share kwa mtu mmoja anayehitaji mwongozo leo.
#FufuaUsikivuWako #1Samweli3 #SautiYaMungu #NenaBwana #Utii #MwongozoWaMungu #VoiceOfHope #VOHOF
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: