MAKOSA 10 YA KIPESA UNATAKIWA KUEPUKA | Michael Kamukulu - LENZI
Автор: LENZI | Michael Kamukulu
Загружено: 2025-04-02
Просмотров: 5262
Описание:
Makosa ya KIPESA Unayopaswa Kuepuka ili Kujenga Uhuru katika uchumi wako binafsi na maisha yako ya kifedha. Jifunze zaidi na Michael Kamukulu kupitia @lenzi.michaelkamukulu
"Utajiri wa kweli hauji kwa bahati, unajengwa kwa maamuzi sahihi ya kifedha na nidhamu thabiti."
Katika video hii, tunajadili makosa ya kifedha ambayo watu wengi hufanya bila kujua na jinsi ya kuyakwepa ili kuimarisha hali ya kifedha kwa muda mrefu. Inawezekana ni katika kuanzisha biashara, matumizi ya familia, matumizi binafsi hata katika kuweka akiba na kufanya uwekezaji.
Mafanikio kifedha ni matokeo ya tabia ya mtu husika katika kutafuta na kupata pesa, kuitunza, kuilinda na kuongeza thamani na uzalishaji wake kifedha.
Moja ya makosa makubwa ni kutegemea mikopo kama njia ya kuendesha maisha ya kila siku kwenye vitu vya kawaida. Mikopo ya kimaendelea, hasa kwenye biashara ni muhimu na inashauriwa kwa wale wanaotafuta maendeleo, lakini tahadhari kubwa inabidi iwepo hasa kwenye ufahamu, nidhamu, mienendo na tabia ya mhusika kwenye maisha yeake ya kifedha.
Watu wengi hujikuta wakikopa ili kugharamia matumizi ya kila siku badala ya kuwekeza kwenye vyanzo vya mapato. Kutegemea mikopo bila mpango mzuri wa urejeshaji kunaweza kusababisha mzigo wa madeni usioisha na kuzuia maendeleo ya kifedha.
Pia, ni muhimu kuhakikisha kuwa matumizi yako hayazidi kipato chako. Watu wengi huanguka kwenye mtego wa kutumia zaidi ya wanavyoingiza, jambo ambalo huwasukuma kwenye madeni au uhaba wa fedha. Hii inahusiana na sheria ya kifedha inayojulikana kama Parkinson’s Law, ambayo inaeleza kuwa matumizi ya mtu yanaongezeka kulingana na kipato chake. Bila nidhamu, mtu anapopata kipato kikubwa, anaongeza matumizi badala ya kuwekeza au kuweka akiba, na matokeo yake ni kwamba hana uhuru wa kifedha licha ya kuwa na mapato makubwa.
Makosa mengine yanayowakwamisha wengi ni kutafuta utajiri wa haraka. Watu huvutiwa na mipango ya kupata pesa kwa muda mfupi, mara nyingi kupitia miradi isiyo na msingi thabiti, ulaghai wa kifedha (scams), au hata uwekezaji wa hatari bila uelewa wa kutosha. Utajiri wa kudumu haujengwi kwa njia za mkato bali kwa nidhamu, uvumilivu, na maamuzi sahihi ya kifedha.
Katika video hii, utajifunza kwa kina jinsi ya kuepuka makosa haya na kujenga msingi imara wa kifedha unaoweza kukupa uhuru wa kweli wa kiuchumi.
🔥 Tazama video hii hadi mwisho ili kufahamu mbinu za kuboresha usimamizi wa fedha zako! 🔥
Usisahau ku-LIKE, KUSHARE, na KUSUBSCRIBE kwa mafunzo zaidi! Na muhimu zaidi, tuambie kwenye comments ni makosa gani ya kifedha umewahi kufanya au unayoyaona kwa wengine!
***
Jifunze jinsi ya kufanya ili uwe tofauti, na upate fursa na nafasi ya kuinuka na kusimama imara ukiwa kiongozi na mwongoza njia wa maisha yako na kuwa na ushawishi kwa watu wengi. Pata maarifa na ujuzi utakaokubadilisha na kuwa na tabia za watu wenye mafanikio na matokeo makubwa kifedha na kimaisha kwa ujumla. Ni wakati wako kung'ara na kuwa mtu wa thamani zaidi kwa wengine na kwa maisha yako. Utajiri na umasikini vyote viko kwenye nguvu ya tabia, mienendo na maamuzi yako ya kila siku.
———————————————
Wasiliana nasi kwa huduma zaidi ikiwemo:
1. Mafunzo na mwongozo maalum wa kufikia malengo (personal/individual coaching)
2. Mafunzo na mwongozo maalum kwa makundi na taasisi (group coaching)
3. Ushauri wa kitaalam kuhusu maendeleo binafsi (personal development)
Mawasiliano yetu:
Simu: +255 752 465 039
Baruapepe: [email protected]
* *
Pata Kozi Kuhusu jinsi ya kujiajiri na kuongeza kipato kwa kutumia MAUDHUI kwa bei nafuu ya TZS 15,000 tu kupitia hapa https://tr.ee/UTrb-ghbfk
#HatuaMojaMbeleKilaSiku #michaelkamukulu #lenzimindset #lenziacademy
Time stamp
00:00 Makosa ya kifedha ya kuepuka
00:14 Usitegemee mikopo
01:06 Matumizi yasizidi kipato
01:48 Usiendeshwe na hisia
02:20 Usitafute utajiri wa haraka
03:03 Usipuuze fursa
03:36 Usitegemee kipato kimoja
04:29 Usikose Mipango na Matumizi
05:16 Usikose Mpango wa kustaafu
06:29 Weka mkazo juu ya elimu ya fedha
07:14 Usipuuze elimu Kodi
07:55 Usikose Akiba
08:53 Usichelewe Kuwekeza
09:30 Closing
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: