Zitto: Wakimbizi Waliopewa Uraia Wana Haki Sawa Kama Raia Wengine
Автор: ACT MEDIA
Загружено: 2024-08-04
Просмотров: 2445
Описание:
Kiongozi mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amemtaka Rais Samia Suluhu kumuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuwaondoa wakuu wa makazi katika kambi za Katumba na Kanoge kwa kuwa wapo kinyume na sheria.
Zitto amesema hayo akizungumza kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika kata ya Ugalla iliyopo jimbo la Nsimbo mkoani Katavi.
Kauli ya Kiongozi huyo imekuja baada ya chama cha ACT Wazalendo kuzuiwa kufanya mkutano wa hadhara katika kambi ya Kanoge wilaya ya Nsimbo, mkoani Katavi Agosti 3, 2024.
Viongozi wa chama hicho wanadai waliandika barua kuomba kibali kwa jeshi la polisi ili kufanya mkutano katika kambi ya Kanoge, lakini walijibiwa na Mkuu wa Makazi wa kambi hiyo kuwa siasa hairuhusiwi eneo hilo.
Kwa mujibu wa Zitto halmashauri ya wilaya Nsimbo ilipokea zaidi ya wakimbizi 200,000 mwaka 1972 kutoka Burundi waliopelekwa katika kambi za Katumba na Kanonge wilayani humo.
Hata hivyo, mwaka 2008 hadi 2010 serikali iliamua kutoa uraia kwa wakimbizi 162,000 waliokubaliwa kuwa raia wa Tanzania
#TaifaLaWote #MaslahiYaWote #miezi10 #wanachamamilioni10
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: