WAJASIRIAMALI KUPEWA KIPAUMBELE SOKO LA CHUINI
Автор: OFISI YA RAIS TAMISEMIM ZANZIBAR
Загружено: 2025-09-01
Просмотров: 1003
Описание:
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Masoud Ali Mohammed amesema wajasiriamali wadogo wadogo watazingatiwa na kupewa kipaumbele mara baada ya kufunguliwa kwa soko la Chuini.
Ameyasema hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua mradi wa soko na kituo cha Mabasi Chuini Wilaya ya Magharib A, kwa lengo la kuangalia maandalizi ya ufunguzi wa Soko na kituo hicho.
Nae Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Magharib A Mohamed Simba Hassan amesema kwasasa wanaendelea na hatua ya kuwapanga na kuwaingiza ndani ya soko Wafanya biashara waliopembezoni mwa barabara huku akitoa wito wa kuwataka wananchi kushiriki katika ufunguzi wa soko na kituo cha mabasi unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Nao wajasiriamali wameeleza matumaini yao kwa kupata soko la kisasa litakalowawezesha kufanya biashara katika mazingia bora na kuiomba serikali kuwapatiwa mikopo ili waweze kukuza biashara .
Soko na kituo cha Mabasi Chuini vinatarajiwa kufunguliwa siku ya Alhamis tarehe 04/09/2025 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Ali Mwinyi.
📆 29 Aug,2025
📍 Chuini, Zanzibar 🇹🇿
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: