WAZIRI KITWANA KUKABIDHIWA RASMI TAWALA ZA MIKOA
Автор: OFISI YA RAIS TAMISEMIM ZANZIBAR
Загружено: 2025-11-20
Просмотров: 16024
Описание:
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Idrisa Kitwana Mustafa amewataka viongozi na watendaji wa wizara hiyo kutoa ushikiano katika utendaji kazi ili kufikia malengo ya wizara iliojiwekea.
Ameyasema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi yaliofanyika katika ukumbi wa ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za smz Vuga mkoa wa Mjini Magharibi.
Amesema matarajio yake ni kuona wizara hiyo inaendelea na utekeleaji wa miradi mikubwa ya kimaendeleo na kuhakikisha wanafikia malengo ya serikali yanafikiwa na kuwafikia wananchi.
Aidha Mhe. Idrisa amesema wizara hiyo inahitaji mashirikiano makubwa kutoka kwa wananchi, mashirika binafsi na Taasisi mbalimbali ili kufanikisha utendaje wake, pamoja na hayo amewahakikishia watendaji wa ofisi hiyo kwamba yupo tayari kupokea ushauri kutoka kwao kwani ndio chanzo cha mafanikio ya ofisi hiyo.
Waziri wa sasa wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Mhe. Masoud Ali Mohammed ambae awali aliku waziri wa wizara hiyo amesema ataendelea kutoa ushirikiano wakati wowote kwani serikali inafanyakazi kwa kutegemeana katika kufikia malengo yaliyowekwa.
Nae katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Issa Mahfoudh Haji amesema wizara imepata kiongozi kutoka katika ofisi hiyo, hivyo anaimani kuongoza vyema Wizara hiyo na kutekeleza majukumu yake.
📆 20 Nov, 2025
📍 Vuga, Zanzibar 🇹🇿
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: