KILIO CHA WAKAZI WA KIPUNGUNI DSM, WAFIKA KWENYE MKUTANO WA DC MPOGOLO NA MABANGO/LEO HAPA HUONDOKI
Автор: JAMBO TV
Загружено: 2024-09-13
Просмотров: 4847
Описание:
Wakazi wa Kipunguni, kata ya Kipawa, wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam wamesema wamechoshwa na ahadi za muda mrefu kutoka serikalini ambapo wakazi hao wanadai fidia zao kufuatia kuachia eneo hilo (Kipunguni) kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)
Jambo TV imeshuhudia kilio cha wakazi hao wakiwemo wanawake na wazee waliokuwa wanawasilisha kero hiyo kwa Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo aliyeitisha mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi, mkutano uliofanyika uwanja wa Banana Wakicha, kata ya Kipawa
Katika maelezo yao wakazi hao wamedai kuwa wamezuiliwa kufanya shughuli zozote za maendeleo kwenye eneo hilo tangu mwaka 1997, hata hivyo kufuatia ukimya wa muda mrefu baadaye serikali ilianzisha mchakato wa kulipa fidia kupitia tathmini ya awali jambo ambalo iliilazimu Mahakama kuingilia Kati na kuiamuru serikali kufanya tathmini upya ili fidia hiyo ilipwe kulingana na thamani ya wakati husika
Akizungumza na wananchi hao Mkuu wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo pamoja na mambo mengine amewaeleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Amesikia kilio chao hivyo ameagiza kuwa wananchi hao walipwe fidia/hela zao haraka iwezekanavyo, na kwamba katika maelezo yake amefafanua kuwa sasa rasmi wananchi hao watalipwa fedha hizo mwezi Oktoba mwaka huu (2024)
Kama haitoshi Mpogolo amezitaka Kamati mbili (2) za wananchi hao walizozichagua kufuatilia jambo hilo tangu mwanzo zifike kwenye ofisi yake (Ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Ilala) Jumanne ya wiki ijayo ili wakapokee taarifa na utaratibu utakaotumika katika malipo na kisha wakirejea wawaeleze wananchi wengine
Katika hatua nyingine Mkuu wa wilaya huyo amewapongeza wananchi hao kwa uvumilivu wao wa muda mrefu wa jambo hilo, sambamba na kuwaleza kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ana mapenzi mema na wananchi hao na ndio maana yuko tayari wakati wote kusikiliza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.
...........
Tufuatilie kwenye mitandao ya kijamii
►YOUTUBE: / @jambotv908
►INSTAGRAM: / jambotv
►TWITTER: / jambotv_
►FACEBOOK: / jambotv
►WEBSITE: https://jambo.tz/
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: