SERIKALI WAPINGA KABENDERA KUMZIKA MAMA YAKE
Автор: Millard Ayo
Загружено: 2020-01-02
Просмотров: 35526
Описание:
Upande wa Serikali umempa pole Mwandishi wa Habari, Erick Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi, Verdiana Mwahuzi huku ikipinga maombi yake ya kutaka ashiriki Ibada ya mazishi ya mama yake.
Hayo yamebainika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati Kabendera anayekabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha alipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kesi yake.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazi, Janeth Mtega kwamba Jamhuri inampa pole Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi.
"Hata sisi tuna masikitiko makubwa na tunampa pole nyingi Kabendera kwa kufiwa na Mama yake mzazi, lakini mahakama isifungwe mikono kwa maombi yaliyowasilishwa ya kutaka kushiriki msiba,"amesema Wankyo.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: