UVCCM GEITA YAKOSOA AJENDA YA DHAHABU YA UPINZANI
Автор: Storm FM Geita
Загружено: 2026-02-01
Просмотров: 59
Описание:
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Geita imevitaka vyama vya upinzani nchini kuacha kushikilia ajenda ya kununuliwa na kuhifadhiwa kwa dhahabu, badala yake vije na ajenda zenye tija kwa wananchi, ikizingatiwa kuwa kwa sasa Taifa lina akiba ya kutosha ya madini hayo.
Kauli hiyo imetolewa mapema leo na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Geita, Manjale Magambo, wakati wa maadhimisho ya miaka 49 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), yaliyoandaliwa na UVCCM Wilaya ya Bukombe na kufanyika katika Kata ya Uyovu.
Magambo amesema tangu Serikali ilipoanza ununuzi wa dhahabu, thamani ya Shilingi ya Tanzania imeimarika huku thamani ya Dola ya Marekani ikishuka, hali ambayo imepunguza kwa kiasi kikubwa uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi.
Kwa upande wake, Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Bukombe, Leonard Mwakalukwa, amesema vijana wa wilaya hiyo wataendelea kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kutokana na mapinduzi makubwa aliyoyafanya katika sekta ya madini.
Nao baadhi ya viongozi wa CCM waliohudhuria maadhimisho hayo wameipongeza Serikali kwa hatua mbalimbali za maendeleo zilizofikiwa, wakieleza kutambua jitihada zinazofanywa na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: