TANGANYIKA DC ILIVYO ADHIMISHA MIAKA 62 YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
Автор: HALMASHAURI YA WILAYA YA TANGANYIKA
Загружено: 2026-01-12
Просмотров: 53
Описание:
Tanganyika DC Staff Bonanza.
Katika kuadhimisha miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imeadhimisha siku hii kwa kuandaa bonanza la michezo mbalimbali lililowahusisha watumishi wa halmashauri hiyo, kwa lengo la kuimarisha umoja, ushirikiano na ujamaa kazini.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Tanganyika, Bw. Clavery Reginald, ambaye aliongoza shughuli hiyo kwa kushiriki michezo pamoja na watumishi.
Katika mchezo wa mpira wa miguu, Timu ya Makao Makuu ya Wilaya ya Tanganyika (Tanganyika HQ) iliibuka mabingwa baada ya kuifunga Timu ya Idara ya Afya kwa mabao 2–0 katika mchezo wa fainali.
Mbali na mpira wa miguu, michezo mingine pia ilifanyika na kupata washindi wake ambapo, katika mchezo wa Draft, Maiko Mbaga aliibuka mshindi wa kwanza, huku Boaz Kutonga akiibuka mshindi wa kwanza katika mchezo wa Karata. Kwa upande wa mchezo wa Ludo, Team Masota ilifanikiwa kushika nafasi ya kwanza.
Bonanza hilo lililenga kuimarisha afya, mshikamano na mahusiano mema miongoni mwa watumishi wa Wilaya ya Tanganyika, sambamba na maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
#Mapinduzi62
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: