RC SHIGELA ATOA NENO KWA WAHITIMU SHULE ZA WAJA
Автор: Storm FM Geita
Загружено: 2025-11-30
Просмотров: 100
Описание:
Mkuu wa mkoa wa Geita Mhe. Martine Reuben Shigela amewataka wahitimu wa kidato cha nne katika shule za WAJA (Wasichana na Wavulana) kuzingatia mafunzo ya kielimu waliyopata kwa miaka minne sambamba na kuishi katika ndoto zao pindi wanaporejea majumbani kwa wazazi wao.
RC Shigela ametoa rai hiyo Novemba 29, 2025 katika sherehe ya mahafali iliyofanyika katika shule ya wasichana ya Waja iliyopo manispaa ya Geita na kusisitiza kuwa hata yeye aliishi katika maono aliyoamini huku akiwa na juhudi na nidhamu.
Mkurugenzi mkuu wa shule hizo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Geita mjini Mhandisi Chacha Mwita Wambura amewashukuru wazazi kwa kuziamini shule za Waja huku akiwasihi wahitimu kuzingatia maadili waliyofundishwa shuleni sambamba na kuwa na nidhamu kwa watu wote kwenye jamii.
Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, mkuu wa shule ya wasichana ya Waja ameeleza kuwa shule hizo zimekuwa zikifadhili wanafunzi tangu 2014 huku akibainisha kuwa miundombinu bora na rafiki imewezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo.
Aidha baadhi ya walimu waliofanya vizuri kwa kuwa na ufaulu mzuri wa wanafunzi kwenye masomo yao wamepewa zawadi ya pikipiki ili kuongeza chachu ya ufundishaji sambamba na kuongeza hari ya ufaulu kwa wanafunzi.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: