RC MTAKA AWACHARUKIA WATENDAJI WA HALMASHAURI KISA TOZO "NASUBIRI TUMALIZE UCHAGUZI, NAFUTA USHURU"
Автор: Millard Ayo
Загружено: 2025-09-26
Просмотров: 1940
Описание:
Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amechukizwa na Urasimu unaofanywa na baadhi ya watendaji wa Serikali wakiwemo wa kwenye mageti ya ukaguzi wanaosababisha hasara kubwa kwa wakulima wa mazao yanayooza kama vile Parachichi na viazi kwa kukaa muda mrefu getini ambapo amesema mara baada ya uchaguzi mkuu kufanyika anakwenda kukutana na wakurugenzi,wakuu wa vitengo na madiwani wote wa halmashauri za mkoa wa Njombe ili kuweza kufuta tozo na ushuru kandamizi kwa wakulima.
Mtaka ameeleza hayo wakati akitoa mwelekeo kwenye kilimo katika mkutano uliokutanisha mikoa nane inayolima Parachichi ili kujadili mstakabali wa zao hilo na kufungua msimu wa ununuzi wa Parachichi ambapo amesema halmashauri ziekuwa zikitoza ushuru wa mazao licha kushindwa kuboresha miundombinu ya kuinua kilimo ikiwemo maji,umeme na barabara.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: