Shamirisho|Yambwa
Автор: Mwalimu Hassan Channel
Загружено: 2020-11-16
Просмотров: 4377
Описание:
Shamirisho /Yambwa
Shamirisho ni jina la kitu au mtu ambalo huathiriwa na kitenzi katika sentensi na huja baada ya kitenzi kikuu.
Aina za Shamirisho
1.Shamirisho kipozi /yambwa tendwa.
Huonyesha kile kinachotendwa katika sentensi; Huonyesha kile ambacho hupokea athari ya kitenzi moja kwa moja. Mfano:Mwalimu anaandika sentensi, Wazazi wanawafunza watoto.
Katika sentensi hizi mbili, sentensi na watoto ni kipozi.
2.Shamirisho kitondo /Yambwa tendewa.
Huonyesha kile ambacho hupokezewa athari ya kitenzi katika sentensi. Mfano :Mama anampikia mtoto chakula, Kibarua alimlimia mkulima shamba.
Katika sentensi hizi mbili, mtoto na mkulima ni kitondo au yambwa tendewa.
3.Shamirisho ala /kitumizi. Huonyesha kile ambacho husaidia kutendeka kwa jambo au kitendo fulani katika sentensi. Mfano :Mama anampikia mtoto chakula kwa sufuria, Kibarua alimlimia mkulima shamba kwa jembe.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: