MWENYEKITI ARUDISHA FEDHA BAADA YA KUBANANISHWA NA TAKUKURU
Автор: SQF TV
Загружено: 2026-03-04
Просмотров: 19
Описание:
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwasi Kusini Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro amerejesha kiasi cha Shilingi milioni mbili laki sita na elfu hamsini (2,650,000) kilichotokana na mauzo ya viwanja vitano vya kijiji hicho, baada ya hatua za uchunguzi na ufuatiliaji zilizofanywa na TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro.
Akizungumza na vyombo vya habari Machi 3,2026 wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa Majukumu wa Taasisi hiyo kwa kipindi Cha mwezi Oktoba hadi Disemba 2025,Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Kilimanjaro Musa Chaulo amesema kuwa uchunguzi uliofanywa na TAKUKURU ulibaini kuwa asilimia 10 ya mapato ya mauzo ya viwanja hivyo, sawa na Shilingi milioni mbili laki sita na elfu hamsini (2,650,000) haikuwekwa kwenye akaunti ya kijiji kama ilivyoamuliwa katika mkutano wa hadhara badala yake fedha hizo zilihifadhiwa nje ya mfumo rasmi wa utunzaji wa fedha za Serikali.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: