MAKATIBU WAKUU WAJADILI HALI YA SIASA KUSINI MWA AFRIKA
Автор: SQF TV
Загружено: 2026-03-06
Просмотров: 6
Описание:
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeongoza kikao cha 12 cha Makatibu Wakuu wa Vyama vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, ambapo pamoja na mambo mengine walijadili hali ya siasa, ukombozi wa kiuchumi na namna ya kuboresha hali za maisha ya wananchi katika nchi zao.
Kikao hicho kilichofanyika leo Machi 6, 2026, Kibaha mkoani Pwani, kilihusisha makatibu wakuu wa vyama sita vya ukombozi Kusini mwa Afrika, ambavyo ni ANC (Afrika Kusini), CCM (Tanzania), FRELIMO (Msumbiji), SWAPO (Namibia), ZANU-PF (Zimbabwe) na MPLA (Angola).
Akizungumza na vyombo vya habari baada ya mkutano huo, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Asha-Rose Migiro, amesema kuwa katika kikao hicho wamepitia maazimio ya mkutano wa wakuu wa vyama hivyo uliofanyika mwaka jana nchini Afrika Kusini.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: