VIDEO: MAAGIZO YA WAZIRI BASHUNGWA KWA MKUU WA JESHI LA POLISI, IGP WAMBURA KUELEKEA SIKUKUU
Автор: ITV Tanzania
Загружено: 2024-12-18
Просмотров: 3630
Описание:
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, kulisimamia Jeshi la hilo kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto barabarani, kuimarisha doria (highway patrol) usiku na mchana pamoja na kuimarisha ulinzi kwenye Nyumba za Ibada katika kipindi cha sikukuu za Christmass na Mwaka Mpya.
Bashungwa ametoa maagizo hayo, wakati akitoa taarifa kwa Umma kuelekea Sikukuu za Mwisho wa Mwaka ambapo amewahakikishia wananchi na Watanzania wote kuwa nchi iko salama.
“Hatuko tayari kuacha tabia za kizembe ziendelee kupoteza maisha ya watu, na wengine kupata ulemavu, huku Sheria za kudhibiti uzembe zikiwa zipo. Tutachukua hatua kali kwa madereva na wasafarishaji wazembe. Ninaomba wasafiri mtupe ushirikiano, na kuunga mkono jitihada hizi, ili tuwe salama tunapokuwa barabarani”amesema Bashungwa.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: