SIDO MOROGORO YAZINDUA MAENEO YA KUFANYIA KAZI VIJANA KUPITIA KONGANI .
Автор: CLOUDS HABARI
Загружено: 2026-02-03
Просмотров: 1
Описание:
SIDO MOROGORO YAZINDUA MAENEO YA KUFANYIA KAZI VIJANA KUPITIA KONGANI .
Shirika la maendeleo ya viwanda vidogo (SIDO) mkoa wa Morogoro limefanya uzinduzi wa maeneo ya kufanyia kazi vijana kupitia Kongani ndani ya mtaa wa viwandani lengo likiwa ni kuwezesha vijana wajasirimali kuwa na maeneo ya kufanyia shughuli zao za ujasirimali
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa SIDO Prof Silyvester Mpanduji ,mkurugenzi wa teknolojia na maendeleo ya viwanda SIDO makao mkuu mhandisi Benedikto Karumuna amesema hatua ya uzinduzi wa maeneo hayo ni utekelezaji wa azma ya rais Dktt Samia Suluhu Hassan ya kuwapatia vijana maeneo ya kufanyia shughuli zao za ujasiriamali na kwamba SIDO imeshatenga maeneo ishirini na tano ya viwanda nchini kwa vijana ikiwemo mkoa wa Morogoro hatua itakayosaidia wajasirimali kuwa na maeneo rasmi na bora ya kuendeshea shughuli za ujasiriamali
Akizindua maeneo ya kufanyia kazi vijana kupitia kongani ndani ya mtaa wa viwandani yaliyopo ofisi za SIIDO mkoa wa Morogoro mkuu wa mkoa Adam Malima ameliagiza shirika la ugavi wa umeme Tanzania (TANESCO) mkoa wa Morogoro kuhakikisha linafikisha umeme katika eneo hilo ili kusaidia uendeshaji wa shughuli za viwanda ambapo kiasi shilingi milipni 94.0 kinahitajika fedha ambazo Tanesco itachangia shilingi milioni 38.0 na SIDO milioni 56.0 ili kufikisha umeme wa KV 500
Moses Ntambi ni meneja wa mfulko wa Self Microfinance mkoa wa Morogoro amesema mfuko huo umepata kiasi cha shilingi bilioni tatu ambazo zitatolewa Kama mikopo kwa wenye sifa na kuwasisitizia wakazi wa mkoa wa Morogoro kuchangamkia fursa hiyo ya mikopo ili kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake Rachel Elisante kutoka taasisi ya Celina Kombani Memorial Foundation akaeleza namna wanavyosaidia vijana ilkiwa ni pamoja na kusaidia watoto na vijana ili kuweza kufikia malengo yao huku wajasiriamali vijana akiwemo mhitimu wa chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Jolenta Joseph anayezalisha bidhaa zitokanazo na mazao ya kilimo ikiwemo viazi lishe, mahindi lishe na maharage lishe pamoja na Kijana anayetengeneza mkaa mbadala Jamanne Mtayomba akaeleza kwa nini wanaendesha shughuli hizo na namna zinavyowasaidia wao kama vijana ,vijana wengine na jamii kwa ujumla katika kukabiliana na changamoto za kilishe na uharibifu wa mazingira na matumizi ya nishati safi.
#Cloudsdigitalupdatesu
#Morogoro
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: