WALIMU HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA WAKABIDHIWA VIFAA VISAIDIZI
Автор: CLOUDS HABARI
Загружено: 2026-01-29
Просмотров: 5
Описание:
WALIMU HALMASHAURI YA WILAYA YA CHUNYA WAKABIDHIWA VIFAA VISAIDIZI
Mkuu wa idara ya elimu ya awali na msingi wilaya ya Chunya mwalimu Marko Busungu amewataka walimu waliopewa vifaa visaidizi katika kutekeleza majukumu yao kuhakikisha wanavitunza vizuri ili viweze kuwasaidia kwa muda mrefu.
Busungu ametoa rai hiyo mapema wakati wa zoezi la kukabidhi vifaa hivyo kwa wahusika ili viweze kuanza kufanya kazi kama serikali ilivyoelekeza huku akiishukuru serikali ya awamu ya sita kipindi cha pili kuwakumbuka walimu wenye mahitaji maalum kwani nao ni watumishi kama watumishi wengine hivyo kuwapatia vifaa kutawapa uhuru wa kufanya kazi lakini pia watajiona nao kuwa sehemu ya jamii wanayoitumikia
Kwa upande wake afisa elimu maalum wa halmashauri ya wilaya ya Chunya Bi. Hawa Mtonyole amesema Halmashauri ya wilaya ya Chunya ina walimu wanne wenye mahitaji maalumu, wawili kati ya hao wamepatiwa vifaa visaidizi kama vile kishikwambi pamoja na kompyuta Mpakato huku walimu wengine wakiendelea kusubiri vifaa hivyo kulingana na uhitaji walio nao.
Kwa niaba ya walimu wengine mwalimu Edward Mwatimba wa shule ya msingi Kibaoni ameishukuru serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ikiongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka watu wenye mahitaji maalum na hatimaye kuwapatia vifaa visaidizi ambavyo vitasaidia wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
@jacqueline_mwangama
#CloudsDigitalUpdates
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: