VIJANA WAVAA MADERA NA KUVAMIA WATU MAJUMBANI
Автор: Kilimanjaro Revival TV
Загружено: 2026-03-06
Просмотров: 33
Описание:
Diwani wa Kata ya Mahida Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro Issack Tarimo ameeleza kusikitishwa na vitendo vya uvunjifu wa amani kwa baadhi ya vijana kuvaa Madera na kujidai ni wanawake na kuvamia watu nyumbani kwao.
Ametoa kauli hiyo Machi 6,2026 mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Rombo katika mkutano wakusikiliza na kutatua kero za wananchi wa Kata hiyo uliyoandaliwa na Mkuu wa Wilaya akieleza kero kubwa ya usalama inayowakabili wananchi wake.
"Lakini watu hao wanaofanya hivyo Mheshimiwa Mkuu wa wilaya wapo na wanajulikana, vijana wachache na wanajidai ni kiburi, kama juzi wameenda kwa mama mmoja wanataka wamnyang'anye fedha ndio mama akapambana, wamemkata mikono mapanga mawili, ni jambo ambalo linahuzunisha na wakati mwingine wanavaa madera kujidai wao ni wanawake ili waweze kuvamia watu majumbani kwao" alisema Tarimo
Aliongeza kusema kuwa "wanajulikana, wamekuwa sugu na wanajidai kwamba hamna chakuwafanya na wakati mwingine hata wazazi wao baadhi yao wanasema watoto wetu wanacheza vikoba vikundi kwakupitia jambo hilo kwahiyo acha wachape kazi,naomba Mkuu wa wilaya kwasababu jambo linapokuwa limekuwa kero kwa wananchi tunaomba ofisi yako mkuu ielekeze watu hawa wafuatiliwe kwasababu wakiwa wameshikwa kwenye matukio ya wizi wanaachiwa baada ya kesi zao labda kuhukumiwa miezi 6 au mwezi mmoja wanarudi hapa na wanaendelea" aliomba Tarimo
Akijibu hoja hiyo Mkuu wa Wilaya hiyo Raymond Mwangwala alimwagiza OCD kumkamata aliyemkata mama mkono na apatiwe taarifa ya kukamatwa kwake kwani serikali ipo kwaajili ya kulinda watu na mali zao.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: