WAUMINI WAASWA KUMGEUKIA MUNGU NA KUMTUMIKIA KATIKA NJIA ILIYOSAHIHI
Автор: Kilimanjaro Revival TV
Загружено: 2026-03-08
Просмотров: 30
Описание:
Mchungaji Msaidizi wa Kanisa la Kilimanjaro Revival Temple, Mch. Wilfred Swai, amewaasa waumini kujifunza kuudhibiti mwili na kuepuka tamaa za dunia ili waweze kuishi maisha yanayompendeza Mungu.
Akihubiri katika ibada ya kwanza kanisani hapo, Mch. Swai alisema kuwa si kila kitu ambacho mwili unatamani kinapaswa kufuatwa na kutimizwa, kwani kufanya hivyo kunaweza kumfanya mtu kupoteza mwelekeo wa maisha ya kiroho.
Alisisitiza kuwa wakati mwingine mtu anapaswa kujiambia wazi kuwa lengo la maisha yake si kutimiza mapenzi yake binafsi, bali kutimiza mapenzi ya Mungu.
“Si kila kitu ambacho mwili wako utakitaka unapaswa kukifanya. Kuna wakati unapaswa kuuambia mwili wako kuwa haupo hapa kutimiza mapenzi yako, bali uko hapa kutimiza mapenzi ya Baba,” alisema Mch. Swai.
Aidha, aliwaonya waumini kuwa kuchagua kuipenda dunia na anasa zake kunaweza kusababisha mtu kupoteza maisha ya milele pamoja na baraka za mbinguni.
Mch. Swai alihitimisha kwa kuwataka waumini kuishi maisha ya kumcha Mungu, kushikamana na mafundisho ya imani na kuweka kipaumbele katika kumtumikia Mungu badala ya kufuata tamaa za mwili na mambo ya dunia.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: