SERIKALI KUIMARISHA UCHUMI WA KIDIJITALI
Автор: ITV Tanzania
Загружено: 2026-02-12
Просмотров: 35
Описание:
Serikali imetangaza kupunguza gharama za leseni na ada za maombi kwa wabunifu, watayarishaji wa maudhui pamoja na vijana wanaotumia majukwaa ya mitandao ya kijamii nchini, ikiwa ni hatua ya kupunguza gharama za uendeshaji na kukuza uchumi wa Kidijitali.
Akizungumza jijini Dodoma katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa Vyombo vya Utangazaji nchini, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, amesema uamuzi huo umetokana na maoni ya wadau wa sekta hiyo waliobainisha changamoto ya gharama kubwa za leseni, na lengo la Serikali ni kuweka mazingira rafiki yatakayochochea ajira kwa vijana, kuongeza ushindani wenye tija na kuimarisha ubora wa maudhui yanayozalishwa mtandaoni.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt. Jabiri Kuwe Bakari, amesema mamlaka hiyo imeanza mchakato wa kuhuisha kanuni ili kuruhusu utangazaji wa redio kwa njia ya kidijitali na kwamba huduma hiyo inatarajiwa kuanza katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya na Dodoma, ikiwa ni sehemu ya maboresho ya sekta ya utangazaji nchini.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: