TAA YATOLEA UFAFANUZI ZOEZI LA UTAYARI LA KUANGUKA KWA NDEGE UWANJA WA JULIUS NYERERE DSM
Автор: Millard Ayo
Загружено: 2025-03-20
Просмотров: 8277
Описание:
Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) imetolea ufafanuzi zoezi la utayari walilolifanya na kuonesha kuwa ndege ilianguka katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi na Kaimu Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege Tanzania, Said Ramadhani Kitanto amesema hilo lilikuwa zoezi maalum la utayari kuona kiwanja cha JNIA kiko tayari kiasi gani katika kukabiliana na majanga na dharura.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa kiwanja cha ndege Kipawa Bi. Bertha Bakwa amesema, zoezi hilo ni juhudi za kuimarisha usalama kwa kukabiliana na majanga na limefanyika kwa mujibu wa taratibu na miongozo ya Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) pamoja na miongozo ya Shirika la Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA).
Pia ameendelea kusema kuwa ikumbukwe kiwanja cha JNIA ni kinara katika Viwanja Afrika kwani kiliweza kupata tuzo ya Usalama iliyotolewa na Baraza la Viwanja vya Ndege Afrika (ACI) Septemba, 2024 hivyo ni wajibu wa Kiwanja kuonyesha kilichopatikana kinathibitishwa kwa umma kwa kuendelea kukifanyia majaribio.
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: