UGUMBA/UTASA (Kukosa mtoto): Sababu, Matibabu
Автор: WikiElimu
Загружено: 2026-02-15
Просмотров: 70
Описание:
Katika video hii inazungumza kuhusu sababu, dalili, matibabu, namna ya kuzuia, matarajio baada ya matibabu ya UGUMBA/UTASA , endelea angalia mpaka mwisho kujifunza
Ugumba (Infertility) ni hali ya kutoweza kupata ujauzito katika kipindi cha mwaka mmoja au zaidi kwa wenzi ambao wamekuwa wakifanya mapenzi bila kutumia njia zozote za uzazi wa mpango. Hali hii inaweza kutokea kutokana na tatizo kwa mwanaume au mwanamke.
• Ugumba umegawanywa katika makundi mawili:
o Ugumba wa awali (primary infertility) - Hawa ni wanandoa ambao wajamiana bila kinga kwa angalau mwaka mzima na hawapati ujauzito
o Ugumba unaotokea baadae (secondary infertility) – Hawa ni wanandoa waliowahi kupata ujauzito angalau mara moja lakini hawajapata mwingine tena baada ya muda mrefu japo wanafanya juhudi za kupata.
Kwa wanandoa walio chini ya umri wa miaka 30 wenye afya njema wanaojamiiana mara kwa mara, wana asilimia 25 - 30% kwa mwezi ya kupata ujauzito.
Mwanamke anafikia kilele cha rutuba ya kuzaa mwanzoni mwa miaka 20. Baada ya umri wa miaka 35 (na hasa 40), nafasi ya mwanamke kupata mimba inapungua sana.
Kushindwa kushika mimba ni jambo linalosababisha hisia kali za uchungu na kujilaumu – sio tu kwa mwanamke – hata mwanaume. Jambo ambalo linasababisha wapenzi wengi kujaribu kutafuta sababu ni nini?
Nini sababu ya ugumba?
Ugumba unaweza kusababishwa na mambo mbalimbali ya kimwili na kihisia. Ugumba unaweza kusababishwa na matatizo kwa mwanamke, mwanaume, au wote wawili.
UGUMBA KWA WANAWAKE:
• Unaweza kutokea kwa sababu ya matatizo kwenye mfumo wa uzazi – ovary hazitoi mayai, mayai yakitolewa yanashindwa kusafiri kwenda kwenye mji wa mimba au kiinitete kikitengeneza kinashindwa kujipandikizwa kwenye mji wa mimba na kukua.
• Sio hayo tu – matatizo mengine ya kimwili pia yanaweza kuchangia – saratani au uvimbe kwenye mji wa mimba, ugonjwa wa kisukari, kufanya mazoezi kupita kiasi, kupata lishe duni, kunywa pombe sana, Uzito mkubwa sana wa mwili, umri mkubwa sana zaidi ya miaka 40, maambukizi ya via vya uzazi (PID), Makovu yanayotokana na magonjwa ya zinaa, homoni pungufu mwilini n.k.
UGUMBA KWA WANAUME:
• Ugumba kwa wanaume unaweza pia kutokea kwa sababu ya matatizo kwenye mfumo wake wa uzazi – manii yanayotengenezwa hayatoshi, yanashindwa kutoka nje au yanakosa ubora unaofaa kutengeneza mtoto.
• Mtatizo haya ya kupungua wingi na ubora wa manii ya wanaume yanasababishwa na sababu zifuatazo:
o Kuzaliwa na matatizo haya ya uzazi - hanithi
o Umri mkubwa (uzee)
o Uchafuzi wa mazingira – plastiki ziko mpaka kwenye maji na zinaathiri manii
o Kukaa katika eneo lenye joto kali kwa muda mrefu
o Matumizi mabaya ya pombe, sigara, bangi au kokeini
o Makovu kwenye mirija inayobeba manii kwa sababu ya magonjwa ya zinaa, upasuaji au kuumia kwenye via vya uzazi
o Homoni kidogo au nyingi sana mwilini
o Matumizi ya madawa fulani, kama vile cimetidine, spironolactone, na nitrofurantoin
Wakati gani utafute matibabu ya haraka?
Ni vizuri mkafanya maamuzi ya kuonana na daktari kama mmejaribu kupata mimba kwa zaidi ya mwaka bila mafanikio.
Utambuzi
Ukifika kwa daktari atachukua historia yako, atakufanyia uchunguzi wa mwili na kuagiza ufanyiwe vipimo.
• Kwa wanawake anaweza kufanya”
o Vipimo vya damu kuangalia viwango vya homoni za uzazi progesterone na homoni za kuchochea mayai kutolewa “Follicle stimulating hormone”
o Anaweza pia, kuingiza kamera ndogo kwenye mji wa mimba na mirija ya uzazi ili kuichunguza (Hysterosalpingography)
o Ultrasound ya nyonga
o Kuchunguza mkojo kuangalia lutenizining hormone (hii hutabiri kama yai limetolewa tayari kwa ajili ya kurutubishwa)
• Kwa wanaume - Kupima ubora na wingi wa manii
Emmanuel Mniko #mniko #wikielimu
Повторяем попытку...
Доступные форматы для скачивания:
Скачать видео
-
Информация по загрузке: